CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE) kimetoa ufafanuzi kuhusu tuhuma za ufisadi zilizotolewa dhidi yake na kudai si za kweli, zinalenga kuharibu sifa za chuo hicho pamoja na uongozi wake.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Mkuu wa chuo hicho,
Profesa Emanuel Mjema alisema kimembaini mfanyakazi wake anayedaiwa
kutoa taarifa hizo katika vyombo vya habari na ametakiwa kujieleza huku
taratibu nyingine zikifuatia.
Mjema
alisema chuo kimesikitishwa na habari hizo zilizochapishwa na magazeti
mawili ya kila siku , zikidai upo ufisadi mkubwa katika chuo hicho.
Alisema
wamekuwa wakifanyiwa ukaguzi na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za
Serikali (CAG) na hakukuwahi kubainika uchafu na kimepatiwa hati safi.
“…niseme
tu tutawashitaki waandishi hawa kwa kutoa taarifa ambazo hazina ukweli
wowote,” alisema Mjema na kusema kimetaka magazeti husika kukanusha
taarifa hizo."



Blogger Comment
Facebook Comment