Meneja
Uendeshaji wa kampuni ya konyagi Bundala Alex Samamba ametunikiwa tuzo
kubwa inayojulikana kama SABMiller Africa Master,tuzo inayotolewa kwa
wafanyakazi wa muda mrefu na waliotoa mchango wa pekee kuendeleza
kampuni na ni moja ya tuzo kubwa na inayoheshimika kwa kampuni hiyo.
Hafla
ya kutunukiwa tuzo hiyo ilifanyika katika mkutano maalumu wa maafisa
mauzo na masoko wa kampuni ya SABMiller uliofanyika mjini Cape Town
nchini Afrika ya Kusini wiki iliyopita na alitunikiwa tuzo hiyo na
Mkurugenzi wa SABMiller wa kanda ya Afrika,Mark Bowman akiwa ni
mtanzania peke yake na mfanyakazi wa kwanza wa kampuni ya Konyagi
kuipata.
Akiongea
muda mfupi baada ya kupata tuzo hiyo Bundala alisema kuwa anawashukuru
wafanyakazi wenzake wote ambao akifanya kazi nao kwa ushirikiano kwa
kuwa mafanikio mara nyingi yanapatikana kutokana na kufanya kazi kwa
bidii na kwa ushirikiano.
“Tuzo
hii japo nimetunukiwa mimi lakini ni kwa ajili ya wafanyakazi wote wa
kampuni ya Konyagi ambao nimekuwa nikifanya nao kazi kila siku na
kukabiliana a changamoto mbalimbali za ushindani zilizopo katika masoko
kwa sasa”.Alisema
Bundala
Alex Semamba akiwa na Mkurugenzi wa SABMiller wa kanda ya Afrika,Mark
Bowman na wafanyakazi wenzake kutoka nchi mbalimbali wakati wa hafla ya
kutunukiwa tuzo.
Anakumbuka
safari mbalimbali alizopitia katika kazi za mauzo ambazo anaeleza kuwa
zinahitaji kuwa mtu mwenye bidii ya kazi na kufanyika kazi ushauri wa
wateja “Pamoja na elimu na nyadhifa nilizoshikilia nilipokuwa kwenye
kazi za usambazaji nilikuwa nafanya kazi pia ya udereva wa malori
makubwa ya kufikisha bidhaa kwa wateja na wakati mwingine kulazimika
kupakua mzigo”.Anasema Alex
Bundala
alijiunga na kampuni ya Konyagi miaka 22 iliyopita katika Idara ya
mauzo na Masoko na kutokana na bidi katika kazi aliweza kupandishwa cheo
kuwa Meneja Masoko na Mauzo anayesimamia kanda mbalimbali.
Kutokana
na umahiri wake katika ubunifu wa mauzo na uendelezaji wa masoko
alipandishwa Cheo kuwa Meneja wa kuendeleza Masoko wa kampuni ambapo
baadaye aliteuliwa kushika nafasi aliyonayo kwa sasa hivi ya Meneja
Uendeshaji wa kampuni.
Bundala Alex Semamba akiwa wafanyakazi wenzake kutoka nchi mbalimbali wakati wa hafla ya kutumiwa tuzo.
Blogger Comment
Facebook Comment