Msimu wa 2015/2016 umemalizika vizuri kwa Barcelona baada ya hapo usiku wa kuamkia leo Jumatatu kushinda Kombe la Copa Del Rey bbaada ya kuipa kichapo cha goli 2-0 klabu ya Sevilla katika mchezo wa fainali.
Magoli yaliyowapa Barcelona ubingwa yalifungwa na Jordi Alba katika dakika ya 97 baada ya dakika 90 kumalizika bila kufungana na mwamuzi Carlos del Cerro kuongeza dakika 30 za muda wa ziada na goli la pili likifungwa na Mbrazil, Neymar.
Aidha timu zote zilimaliza mchezo huo wa fainali zikiwa na wachezaji nusu baada ya Mascherano kwa upande wa Barcelona kuonyeshwa kadi nyekudu dakika ya 36 na upande wa Sevilla wachezaji wake Ever Banega dk. 90 na Daniel Carrico katika dakika ya 120.
Ubingwa huo kwa Barcelona umekuwa wa pili kwa msimu huu baada ya kushinda kobe la Ligi Kuu ya Hispania(La Liga).