Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(kushoto),
Flaviana Matata na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na
Muungano January Makamba wakiweka shada la maua kwenye kaburi la pamoja
ikiwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 ya kumbukumbu ya kuzama kwa
meli ya MV. Bukoba.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye pamoaja na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January
Makamba wakijiandaa kuwasha mishumaa.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(kushoto)
akiweka mshumaa kwenye kaburi pamoja na Flaviana Matata kwenye
maadhimisho ya miaka 20 ya kuzama kwa MV. Bukoba ambapo mamia ya watu
walipoteza maisha.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(kulia)
akimsikiliza Flaviana Matata muda mfupi kabla ya kupiga picha ya pamoja
za kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 20 ya kuzama kwa meli ya MV.
Bukoba.
Picha ya Pamoja.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza
wakati wa kuangalia mazoezi ya uokoaji majini yaliyofanywa na vijana 50
waliohitimu mafunzo ya uokoaji yaliyodhaminiwa na Flaviana Matata
Foundation pamoja na UTT wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 20
tangia kuzama kwa meli ya MV. Bukoba yaliyofanyika mjini Mwanza ambapo
mamia ya watu walifariki akiwemo mama mzazi na binamu wa Flaviana
Matata.
Sehemu
ya waliofuzu mafunzo ya uokoaji wakionyesha namna ya kuokoa watu majini
wakishuhudiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Nape Nnauye, Mhe. January Makamba Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe.
Stanslaus Mabula na Flaviana Matata
Sehemu
ya makaburi ya pamoja ya waliofariki kwenye ajali ya MV. Bukoba mwaka
1996 ambapo leo imetimia miaka 20 tangia ajali hiyo imetokea.
Viongozi wa Dini walioshiriki kwenye kutoa ibada maalum ya kumbukumbu ya miaka 20 tangia kutokea kwa ajali ya MV. Bukoba.
Blogger Comment
Facebook Comment