Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako Avunja Bodi ya TCU kwa kupitisha Majina ya Wanafunzi Wasio na sifa za Kusomea Shahada


Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amevunja Bodi ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), baada ya kubaini kuwa Tume hiyo ilipitisha majina ya wanafunzi 486 wasio na sifa kusomea Shahada ya Elimu.

Profesa Ndalichako ametangaza uamuzi huo leo ikiwa ni pamoja na kuwasimamisha kazi baadhi ya Maafisa wa Tume hiyo waliobainika kushindwa kutekeleza wajibu wao.

Kutokana na uamuzi huo, Profesa Ndalichako amewateua maafisa wengine watakaokaimu nafasi hizo zilizoachwa wazi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment