Watuhumiwa 711 Wakamatwa Dar es Salaam


Kamanda wa polisi kanda maalumu  Dar es salaam Simon .N. Sirro amesema jumla ya watuhumiwa 711 wa makosa tofauti tofauti wamekamatwa kati ya siku ya juma tatu mpaka Alhamisi usiku wiki hii.

Akitoa taarifa kwa wanahabari leo tarehe 11 Kamanda Sirro amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya unyang’anyi wa kutumia nguvu, kukutwa na bhangi na gongo kucheza kamari,biashara za kuuza mwili pamoja na kubugudhi abiria.

Aidha kamanda Sirro amewataka wenyeviti wa mitaa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kwamba maeneo yanayowazunguka yanakuwa shwari kwa kuhakikisha hakuna biashara haramu zinazoendelea za kusababisha uhalifu.

Hata hivyo ametaja maeneo yanayoongoza kwa kuwa na wauzaji wa bangi na gongo katika maeneo ya Dar es salaam ni Kawe  na Mabibo na kueleza kuwa operesheni maalumu itaendelea kufanyika kila siku kuhakikisha mitaa inakuwa safi.

Ameongeza kwamba kwa sasa pia vijana wajulikanao kama panya road nane wamekamatwa na kudai kuwa wanatumiwa kufanya matendo ya ki uhalifu na tajiri mfanyabiashara wa kariakoo jijini Dar es salaam
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment