NA BEATRICE LYIMO-MAELEZO
Chama cha mpira wa Kikapu Dar es
salaam (RBA) kimeanzaa mashindano ya ligi ya mpira huo
yatakayoshirikisha timu 16 kutoka kwa wananume na timu nane za wanawake.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa chama hicho Okare Emesu alisema
kuwa ligi hiyo inatarajiwa kuanza Januari 28 mpaka julai 30 mwaka huu.
Alisema kuwa viongozi wa RBA
wamekuja na mikakati hiyo ili kuleta chachu kwenye maeneo mengine ya
mkoa, ligi ya watoto chini ya miaka 14, ligi ya daraja la kwanza, ligi
ya vyuo, ligi ya mashirika, ligi ya mashule, program maalumu kwa ajili
ya kukuza vipaji kwa mpira wa kikapu nchini.
“Tangu kuanzishwa kwa chama hiki,
kumekuwa na mafanikio ya muda mfupi ikiwemo ushiriki kwenye mashindano
ya Taifa na kushika nafasi ya pili kwa wanaume na wanawake jambo ambalo
halikuweza kufanyika kwa takribani miaka mitatu sasa” Alisema Mwenyekiti
huyo.
Aidha akizungumzia kuhusu mfumo wa
ligi utakaotumika kwenye mashindano hayo, Mkurugenzi wa Mawasiliano na
Masoko RBA Peter Mpangala alisema kuwa mfumo utakaotumika ni mfumo wa
nyumbani na ugenini katika hatua za awali na timu nane za wananume za
nafasi za juu zitacheza mtoano hadi kupata bingwa.
Mbali na hayo alisema kuwa
kutakuwa na maonyesho ya awali ya ligi ya RBA (Pre RBA Show case) siku
ya Mapinduzi januari 12, mwaka huu kwenye viwanja vya mpira wa kikapu
vya Gymkhana yakilenga kukaribisha wadau mbalinmbali kuona mfano wa ligi
ya RBA itakavyokuwa.
Timu zinazotarajiwa kushiriki
kwenye ligi hiyo kwa upande wa wanaume ni JKT, Mgulani, Ukonga Kings,
Magereza, Savio, Pazi, DB Youngstars, Magnet, ABC, Mabibo Bullets,
Outsiders, Kurasini heat, Oilers, Vijana, Chui na Jogoo na kwa upande wa
wanawake ni JKT Stars Jeshi Stars, Vijana Queens, DonBosco Lioness,
Ukonga Queens, Kurasini Divas na Oilers Princess.
0 comments :
Post a Comment