Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana July
29 2016 alianza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida, Tabora,
Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma ambapo alizungumza na wananchi
kwa lengo la kuwashukuru kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa
mwaka jana na kueleza juhudi zinazofanywa na serikali katika kutatua
kero za wananchi na kuwaletea maendeleo.
Akizungumza
na wananchi wa Manyoni mkoani Singida Rais Magufuli alizungumzia kuhusu
wabunge wa upinzani kususia bunge kwa kujiziba midomo na makaratasi
Alisema
wabunge hao wa upinzani waliamua kususia bunge kwa sababu kilichokuwa
kikijadiliwa ndani ya bunge ni mahakama ya mafisadi na wao (wapinzani)
ni sehemu ya mafisadi .
"Hawakuingia
kwenye bunge kwa sababu walijua ni part ya hao mafisadi, nataka nieleze
hawatapenya mbele ya serikali yangu, mafisadi lazima wanyooke" Alisema Rais Magufuli



Blogger Comment
Facebook Comment