Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema askari wake bado wako katika mapambano ya kukabiliana na wanaotuhumiwa kuwa majambazi katika msitu uliopo maeneo ya Vikindu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam .
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Kamishna wa Kanda hiyo Simon Sirro, amesema operesheni hiyo imeanza kuanzia juzi na inatarajiwa kumalizika siku ya jumanne ijayo na kwamba maeneo yatakayopitiwa na operesheni hiyo ni pamoja na Vikindu, Pwani na Dar es Salaam.
“Tulikuwa na operesheni jana kule vikindu baada ya mauaji ya askari 4 yaliyotokea siku kadhaa zilizopita huko Mbande, raia wema wametoa taarifa zinazohusiana na mauaji hayo na tunazifanyia kazi,” amesema na kuongeza.
“Katika operesheni hiyo watu kadhaa wamefariki dunia, watu kadhaa wamekamatwa na kwamba operesheni inaendelea hadi sasa kwenye msitu,”
Kamanda Sirro amesema hawezi akatoa taarifa za ndani za opereaheni hiyo kwa sasa sababu ni kinyume cha sheria na pia inaweza ikaathiri operesheni hiyo.
“Itakuwa ni kinyume cha utaratibu nikieleza kinachoendelea kwenye operesheni, niwahakikishie silaha zilizochukuliwa zinarudi,kinachoendelea nitawajulisha jumanne ili wananchi wajue kitu gani kinaendelea,” amesema.
Ameongeza kuwa “Mapambano ni ya kawaida sana, na ndio maana aakari polisi akifa kwa silaha ni jambo la kawaida sana. Operesheni tutaifanya maeneo ya Vikindu, Pwani Dar es Salaam, sababu hii network (mtandao) ipo na lazima tutaisafisha kama walidhani wataitawala DSM wamejidanyanya lazima tutarudisha heshima ya jiji.”
Katika hatua nyingine, Sirro amesema amepata taarifa kuwa wapo baadhi ya watu wanapewa fedha kwa ajili ya kufanya maandamano Septemba Mosi mwaka huu ambapo ametoa onyo kwa watakaoshiriki kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria kwa kuwa maandamano hayo hayajaruhusiwa.
“Wote tunajua madhara ya fujo, wazalendo naomba msishiriki, Wanaotaka kujionesha wanapambana na polisi waje barabarani, ” amesema.
Aidha, Sirro amewatoa hofu wananchi wa Dar es Salaam kuwa jiji liko shwari na kwamba hali ya usalama itarejea kama ilivyokuwa awali.
Na Regina Mkonde
Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro akizungumza na wanahabari (Hawapo pichani) muda huu wakati wa kutoa taarifa ya kuongeza kikosi cha askari 80 kwenda kwenye mapambano huko Vikindu..
Baadhi ya askari wakiwa tayari kwenye magari yao wakati wa kujiandaa kuelekea Vikindu kwenye mapambano
Vikosi hivyo vikitoka makao makuu ya kanda maalum ya Dar kuelekea kwenye mapambano muda huu
Vikosi maalum vikielekea kwenye mapambano muda huu
Vikosi vikiwa tayari tayari kuelekea kwenye mapambano muda huu. mtandao wa huu wa Modewjiblog utaendeelea kukupatia taarifa mbalimbali kutoka kwenye eneo la tukio kadri tutakavyozipata.
0 comments :
Post a Comment