1. Katika
kikao chake cha tarehe 05 Septemba 2016, pamoja na mambo mengine,
Kamati Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo iliazimia kuwa Chama kifanye
Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia (National Democratic Congress) tarehe 24
Septemba 2016 jijini Dar es Salaam.
2Tangu
kutangazwa kwa umma kuhusu mipango ya kufanyika kwa mkutano huu,
wanachama wetu wengi na wananchi kwa ujumla, wakiwemo baadhi kutoka
mikoani wameonesha nia ya kushiriki. Ili kuwapa fursa viongozi,
wanachama na wananchi kushiriki kwenye mkutano huu, Chama kimesogeza
mbele tarehe ya kufanyika kwake hadi tarehe 08 Octoba 2016.
3. Wanachama na wananchi ambao wangependa kushiriki kwenye mkutano huu watume majina yao na majimbo wanayotoka kwa namba 0653619906/0717047574.
Ili kutoa muda wa kutengeneza vitambulisho vya washiriki, siku ya
mwisho ya kupokea majina ya washiriki ni tarehe 01 octoba 2016.
4. Ikumbukwe
kuwa mbali na kujadili masuala mbalimbali ya nchi na bara la Afrika,
Mkutano wa Kidemokrasia ndiyo fursa pekee ya kikatiba ambapo
mwanachama/mwananchi wa kawaida anayeshiriki anapata fursa ya kuwahoji
ana kwa ana viongozi wa kitaifa wa ACT Wazalendo juu ya masuala
mbalimbali ya Chama.
Ado Shaibu
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma
Imetolewa leo tarehe 21 Septemba 2016.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments :
Post a Comment