Vijana
wametakiwa kuienzi na kuendelea kuitunza amani iliyoachwa na waasisi wa
taifa ili kuijenga Tanzania yenye amani na utulivu kwa mustakabali wa
kizazi cha sasa na baadaye.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph
Warioba wakati wa ufunguzi wa Mhadhara wa Tatu wa Mwalimu Nyerere
uliojadili maendeleo ya elimu ya juu Afrika ulioambatana na ufunguzi wa
hifadhi ya nyaraka ya Mwalimu Nyerere.
Jaji
Warioba alisema kuwa vijana wanatakiwa kuenzi na kuendeleza amani
iliyoachwa na waasisi wetu kwa kuwa imejenga misingi bora katika kwa
vizazi vya Watanzania.
“Vijana
ni nguvu kazi ya taifa hivyo mnapaswa kuitunza na kuendeleza amani
ambayo imeachwa na waasisi wa taifa kwa maendeleo ya nchi yetu,” amesema
Jaji. Warioba.
Aidha
Jaji Warioba alisema kuwa vijana waache kutumia muda wao kuzungumzia na
badala yake watumie nguv na akili kufanya maendeleo yao na ya jamii kwa
ujumla ili kuijenga nchi.
Kwa
mujibu wa Jaji Warioba alisema kuwa vijana wanapaswa kuwa mstari wa
mbele katika kuimarisha umoja na mshikamano ili kuondokana na ubaguzi wa
rangi, kabila, vyama vya siasa na dini na kupigana na maadui watatu wa
umasikini, ujinga na maradhi.
Mbali
na hayo Jaji Warioba aliwataka kuwa wanasiasa nchini kuwa msaada mkubwa
wa wananchi badala ya wananchi kugeuka msaada kwa wanasiasa.
Na Ally Daud- MAELEZO


0 comments :
Post a Comment