CHAMA cha Wananchi (CUF), kimegomea hatua ya
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, ya kumrudishia
madaraka ya uenyekiti wa chama hicho taifa, Prof. Ibrahim Lipumba.
CUF ilitoa msimamo wa kumpinga Msajili jana ikiwa muda mfupi baada ya taarifa za kurudishwa kwa Lipumba madarakani kuwafikia.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro, alisema kuwa yuko kikaoni, lakini baadaye akafafanua juu ya msimamo
wao kupitia ujumbe mfupi wa maneno kuwa, kamwe hawatambui uamuzi huo
kwa sababu kwa katiba yao na kwamba Msajili wa Vyama vya Siasa hana
mamlaka ya kumrudisha Lipumba kwenye nafasi hiyo.
Mtariro alisema wanachojua ni kwamba jambo pekee analoweza kulifanya Msajili ni kukishauri chama juu ya masuala mbalimbali ya uendeshaji na si kuwawekea mtu wa kuwaongoza.
“Msajili hana mamlaka hayo. Anachoweza kutoa ni maoni tu,” alisema Mtatiro kupitia ujumbe huo mfupi wa simu yake ya mkononi.
0 comments :
Post a Comment