
Kufuatia mauaji ya mwanahabari Daud Mwangosi, Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini, UTPC ulitenga Septemba 2, kuwa kumbukumbu ya Kifo cha Daudi Mwangosi ikiambatana pia na tuzo inayotolewa kwa mwanahabari aliyefanya kazi katika mazingira magumu ikiwemo kupigwa ama kuuawa kutokana na kazi yake.
Jana UTPC imekutana na wanahabari Jijini Mwanza na wanahabari ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kifo cha Mwangosi ambapo imelaani mazingira magumu ambayo wakati mwingine wanahabari na vyombo vya habari wanayapitia katika utendaji wao wa kazi ikiwemo vyombo vya habari kufungiwa.
Makamu wa Rais wa UTPC, Jane Mihanji (kushoto) amesema wanahabari wanataka mazingira huru ya kufanya kazi huku akilaani serikali kuvifungia baadhi ya vyombo vya bila kusikilizwa juu ya yale yanayodhaniwa kufanywa na vyombo hivyo kinyume cha sheria.
Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan, amebainisha kwamba tunzo ya Daudi Mwangosi mwaka huu pia haikupata mshindi kwa namna ambavyo jopo la tuzo hiyo lilivyoweka vigezo vyake ikiwemo Mwandishi anayepaswa kuichukua awe amepigwa, kuumizwa ama kuuawa akiwa kazini. Mwaka 2013 tuzo hiyo ilichukuliwa na Mwanahabari Absolum Kibanda.
( Picha ya kulia akiwa na aliyekuwa DC wa Kilolo, Bw. Mfutakamba, niliipiga enzi za uhai wa Mwangosi.
0 comments :
Post a Comment