CHADEMA:Serikali Ya Magufuli Haifuati Utawala Wa Sheria Kila Mtu Anafanya Maamuzi Anavyojisikia.


Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Ruth Mollel ameikosoa Serikali akidai imekithiri kwa ukiukwaji wa sheria za utumishi.


Katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari jana, Mollel ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya Chadema, amesema ameshuhudia ukiukwaji mkubwa wa Sheria ya Utumishi wa Umma ya Mwaka 2002 kuhusu suala la nidhamu kwa watumishi tangu Serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli iingie madarakani.  

“Tumeshuhudia baadhi ya viongozi wa kisiasa kama mawaziri, naibu mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya wakiwawajibisha watumishi ilhali hawana mamlaka hayo kisheria,” amesema
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment