Serikali imepiga marufuku viwanda kuzalisha mifuko ya platiki kuanzia Januari mwakani.
Akizungumza
na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira mjini
hapa jana, Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira, Richard Muyungi amesema
wanachosema wabunge hakina tofauti na kilichoandikwa kwenye kanuni
zinazoandaliwa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa uamuzi huo.
“Sisi
katika kanuni zetu tumewapa miaka miwili ya kubadilisha teknolojia hiyo
kwenda katika uzalishaji wa mifuko inayooza ili kuepuka athari za
mazingira,” amesema Muyungi.
Amesema mwaka 2013 walisitisha kusajili viwanda vya kuzalisha mifuko ya plastiki ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira.



0 comments :
Post a Comment