Kuelekea
mchezo wa EPL kati ya Chelsea ambayo inataraji kuwe mwenyeji wa
Manchester United, mchezo utakaopigwa katika kesho jumapili katika dimba
la Stamford Bridge, kocha wa Manchester United amezungumza kuhusu
mchezo huo.
Mourinho
ambaye aliondoka Chelsea msimu uliopita baada ya kupata matokeo ambayo
hayakumfurahisha mmiliki, Roman Abramovich na mashabiki wa klabu,
amesema anakwenda katika mchezo huo akiwa ameshakua na kilichomtokea
Chelsea hakiwezi kumtokea kwa mwaka wake wa kwanza akiwa na Man United.
“Muda
umewadia nikiwa nimeshakua, nikiwa meneja imara. Nina hisia imara, sio
mtoto. Haiwezi kutokea kwa mwaka wa kwanza katika historia yangu ya kazi
ya umeneja,
“Nina
furaha kuwa na klabu kubwa kama Manchester United katika maisha yangu
ya kazi sio kwa miezi mitatu iliyopita, lakini naweza kusema katika
mashindano [Ligi Kuu ya Uingereza] ambayo ndiyo ninayoipenda zaidi,”
alisema Mourinho.
Aidha
Mourinho alizungumza kuhusu uhusiano wake na mmiliki wa Chelsea, Roman
Abramovich ambaye amewahi kuwa bosi wake wakati akifundisha Chelsea na
kusema kuwa hakuwa rafiki yake na wala hakuwa mtu wake wa karibu.
“Ni
uhusiano wa mmiliki na meneja, tuliheshimiana sana. Hakuwahi kuwa
rafiki yangu, na wala hatukuwa na ukaribu baina yetu,” alisema Mourinho.


0 comments :
Post a Comment