Mbowe kuiburuza Serikali mahakamani



Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema ataiburuza Serikaliya Awamu ya Tano mahakamani ili chombo hicho cha haki kitoe tafsiri ya vitendo vya ukandamizaji wa demokrasia vinavyofanywa na viongozi wa Serikali hasa Mkoani Arusha.

Mbowe ameyasema hayo alipokuwa akilaani kitendo cha Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, kuwasweka selo madiwani wanne wa chama hicho akisema kuwa hiyo ni ishara ya kwamba utawala wa awamu ya tano hauheshimu sheria.

“Nimewaagiza wanasheria wangu kwenda mahakamani ili kupata tafsiri sahihi kuhusu vitendo hivyo,” amesema.

Ameongeza kuwa viongozi hao wamekuwa wakifanya vitendo vya udhalilishaji kwa baadhi ya wabunge, madiwani, mameya na wenyeviti wa halmashauri kinyume na sheria.

“Nawashangaa sana Wakuu wa Mikoa na Wilaya wamekuwa wakiwadhalilisha wawakilishi wa wananchi ilhali wao wakiwa ni waajiriwa ambao hawajaomba kura kwa wananchi. Jambo hili limeanza mwaka huu, na hii ni nafasi mbaya sana kwa Rais Magufuli kuchagua makada badala ya watumishi,” amefunguka Mbowe.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment