
Kaimu
Meneja Mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es Salaam,
Mhandisi Iddi Rashidi, akizungumzia kukamilika kwa ujenzi wa mfumo wa
njia ya kusafirisha umeme ardhini, (Underground Transmission Lines),
kwenye shule ya sekondari ya wasichana Jangwani jijini Dar es Salaam,
Oktoba 22, 2016.

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
SHIRIKA
la umeme nchini (TANESCO), limekamilisha ujenzi wa mfumo wa njia ya
usafirishaji umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission Lines) ,
kutoka shule ya sekondari ya wasichana ya Jangwani jijini Dar es Salaam
na kutoka kituo cha umeme cha Makumbusho kwenda kituo kipya cha kupozea
umeme kilichoko katikati ya jiji cha City Centre cha ukubwa wa 100MVA
(2X50MVA), 132/33KV.
Akizungumzia
maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme
jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Iddi Rashidi,
alisema, kukamilika kwa ujenzi wa mfumo huo ambao utahusisha ujenzi wa
mfumo wa njia za usambazaji umeme chini ya ardhi (Underground
Distribution Lines), wa kilomita 4.3 wa msongo wa kilovolti 33 kwa ajili
ya kuunganisha kituo cha City Centre na vituo vingine vitatu vya
Kariakoo, Railway na Sokoine.
Akifafanua
zaidi, Mhandisi Rashidi alisema, ujenzi wa mfumo wa njia ya
usafirishaji umeme chini ya ardhi (Underground Transmision Lines), kwa
msongo wa Kv132 kutoka Makumbusho kwenda kituo cha City Centre tayari
umekamilika na ule wa kutoka shule ya sekondari ya wasichana Jangwani
kwenye City Centre pia umekamilika.
“Faida
kubwa ambayo wakazi wa jiji la Dar es Salaam watarajie ni kupata umeme
wa uhakika (reliable power supply ulio kwenye viwango stahiki,
(Acceptable quality power supply) hususan kwa wale wa maeneo ya katikati
ya jiji,” Aliongeza Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ilala, Mhandisi
Athanasius Nangali.
Akieleza
zaidi, Mhandisi Nangai alisema, “Mradi huu unaviwezesha viituo tajwa
kuwa na njia mbili za kuvvipatia umeme na hivyo kuwezesha kuwa na njia
mbadala ya kupata umeme endapo njia moja kati ya hizo itakuwa na
hitilafu.” Alifafanua.
Alisema
kuongezeka kwa kituo cha City Centre cha 100MVA, kunafanya jiji la Dar
es Salaam pekee kuwa na jumla ya vituo 9 vya aina hiyo. “Hivi sasa
tunaweza kusema, ujenzi umekamilika kwa zaidi ya asilimia 98,
kinachoendelea ni kukamilisha ujenzi wa mfumo wa njia ya kusafirisha
umeme kupitia juu (Overhead Transmission Lines), wa kilomita 1.3 wa
msongo wa kilovolti 132 kutoka kituo kikubwa cha kupozea umeme cha Ilala
hadi shule ya sekondari ya wasichana Jangwani ambapo utaungana na mfumo
wa usafirishaji umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission Lines)
kwenda kituo kikubwa cha City Centre.” Alifafanua.
kutoka
Makumbusho kwenda kituo cha City Centre, umekamilikakatikati yan jiji
utekelezaji wa Mradi huo, unaofadhiliwa kwa pamoja na Serikali ya
Tanzania na Finland, unahusisha ujenzi wa kituo cha udhibiti mifumo ya
usambazaji umeme (Distribution SCADA System), katika msongo wa kilovolti
33 na 11.
“Tayari
ujenzi wa kituo cha City Centre umekamilika kwa asilimia 100 na sasa
tuko katika hatua za majaribio.” Alisema Mhandisi Rashidi.
Naye
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, amewaomba wakazi wa
jiji kuwa wavumilivu wakati zoezi hili la kuboresha miundombinu
likiendelea kwani huwa panatokea kukatika kwa umeme sehemu Fulani Fulani
ili kutoa nafasi kwa mafundi kufanya kazi kwa usalama zaidi.(P.T)
Meneja
wa TANESCO Mkoa wa Ilala, Mhandisi Athanasius Nangali, (kulia), akiwa na
Kaimu Meneja Mradi, Mhandisi Iddi Rashidi wakati wakizungumza na
waandishi wa habari kuhusu mradi huo

Meneja
wa TANESCO Mkoa wa Ilala, Mhandisi Athanasius Nangali, (katikati),
Kaimu Meneja Mradi, Mhandisi Iddi Rashid, (kulia), Afisa Habari na
Mawasiliano wa TANESCO, Hendry Kilasila, wakitembelea eneo la ujenzi wa
Mfumo huo shule ya sekondari Jangwani jijini Dar es Salaam

Hizi ndio njia za kusafirisha umeme ardhini zilizojengwa kwenye shule ya sekondari ya wasichana Jangwani jijini Dar es Salaam

Nguzo ya
kusafirisha umeme wa juu kutoka Kituo cha Ilala kuja shule ya sekondari
ya wasichana Jangwani, ambapo zitaungana na Mfuko wa njia ya
kusafirisha umeme ardhini kupelekea katikati ya jiji


Mafundi wakiwa kazini



Mhandisi Nangali, (mbele), Kaimu Meneja Mradi, Mhandisi Rashid, (kulia), wakiangalia moja ya roller lenye nyaya.


0 comments :
Post a Comment