Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi
Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Bibi Leah Kihimbi (wa tatu kushoto waliokaa) akiwa katika
picha ya pamoja na Viongozi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
(TaSUBa) pamoja na wahitimu wa ngazi ya Stashaha katika sherehe za
mahafali ya 27 ya Chuo cha Ufundi na Sanaa Bagamoyo kilichopo chini ya
Taasisi hiyo .Wa kwanza Kulia Mkuu wa Idara ya Elimu ya Taasisi hiyo na
Wa pili kulia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
Dkt.Herbet Makoye.
………………………………………………………………..
Na Shamimu Nyaki- WHUSM.
Katika kukabiliana na upungufu wa
ajira hapa nchini Vijana wameshauriwa kujiajiri kupitia Sanaa na
vipaji walivonavyo katika kupata kipato.
Ushauri huo umetolewa jana
Wilayani Bagamoyo na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa
kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi Leah Kihimbi
alipokuwa anawahutubia wahitimu wa Astashahada na Stashahada ya Sanaa
na Ufundi katika Chuo cha Sanaa na Ufundi Bagamoyo kilichopo chini ya
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).
“Tumieni elimu mliyopata
kujiajiri wenyewe ili kuepuka changamoto ya ajira iliyopo hapa nchini,
ujuzi mliopata ni njia pekee ya kujiletea kipato na Taifa kwa
ujumla”.Alisema Bibi Leah.
Aidha Kaimu Mkurugenzi huyo
aliongeza kuwa wasanii wote wanaofanya kazi za Sanaa ni vyema
wakasajili kazi zao katika Mamlaka husika ili iwe rahisi kwa Serikali
kutoa msaada kwa urahisi kwaWasanii hao.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu
waTaasisi ya Sanaa na Utmaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt.Herbet Makoye
aliwasihi wahitimu hao kuwa mabalozi wazuri wa sanaa watakapokuwa
wanafanya shughuli zao za Sanaa.
“Nendeni mkawe mabalozi wazuri
wa Chuo chetu kwa kuwa Wasanii bora na kutengeneza kazi nzuri ili
muweze kushindana na soko la ajira”. Alisisitiza Dkt.Makoye.
Naye mhitimu wa ngazi ya
Stashahada ya Sanaa na Ufundi Bi Imelda John amesema kuwa elimu
aliyoipata itamsaidia kufanya kazi ya Sanaa kwa weledi zaidi hasa
katika fani ya kutengeneza Filamu na Picha Jongefu.
Mahafali hayo ni ya 27 katika
chuo hicho ambapo kwa mwaka huu jumla ya wanafunzi 85 wametimu
Astashahada na Stashahada ya Sanaa na Ufundi.


0 comments :
Post a Comment