Klabu ya Arsenal ipo katika hatua nzuri ya kukamilisha mpango wa
kuwasainisha mikataba mipya wachezaji wake Alexis Sanchez na Mesut Ozil
chini ya ushawishi mkubwa unaoendelea kufanywa na meneja Arsene Wenger.
Taarifa zinasema kuwa, Wenger amependekeza wawili hao wasainishwe
mkataba wa miaka miwili, ambayo itakua chachu ya kuanza kulipwa
mishahara minono kutokana na kazi nzuri na kubwa wanayoifanya kwa ajili
ya maendeleo ya Arsenal tangu walipotua klabuni hapo.
Mwishoni mwa juma lililopita Wenger aliwaeleza waandishi wa habari
“Tupo tayari kuvunja benki kwa ajili ya kukamilisha mpango wa kusainiwa
kwa mkataba mpya wa Ozil ambao utamuwezesha kupokea mshahara wa Pauni
250,000 kwa juma.”
Hali kadhali kauli kama hiyo aliitoa alipoulizwa kuhusu maendeleo ya mazungumzo kati ya uongozi wa Arsenal na Sanchez.
Wenger kwa sasa anamalizia muda wa mwaka mmoja uliosalia kwenye
mkataba wake, lakini amekua na matumaini makubwa ya kuwabakisha
wachezaji hao klabuni hapo kwa ajili ya maslahi ya baadae.



0 comments :
Post a Comment