Mshambuliaji wsa Taifa Stars,
Elius Maguri akichuana na beki wa Zimbabwe, Hadebe Teenage katika mchezo
wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe leo.
Tanzania ilifungwa mabao 3-0.
………………………………………………………………………………
Na.Alex Mathias.
Timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’
imeshindwa kutamba ugenini dhidi ya wenyeji Zimbabwe ‘The warriors’
baada ya kukubali kufungwa magoli 3-0 mchezo wa kirafiki wa kimataifa
uliochezwa uwanja wa Harare nchini Zimbabwe.
Dakika ya 7 Zimbabwe aliwapata goli la
kwanza likifungwa na mshambuliaji hatari,Knowledge Musona anayecheza
klabu ya KV Oostende ya Ubelgiji baada ya mpira uliopigwa na Mathew
Rusike na Erasto Nyoni alishindwa kuokoa mpira huu na kumkuta mfungaji
katika sehemu nzuri ya kufunga.
Baada ya kufungwa goli hilo vijana wa
Mkwasa waliendelea kulisaka lango la wenyeji na katika dakika 25 Samatta
alikosa goli la wazi akiwa peke yake na golikipa na dakika ya 27 Simon
Msuva alioneshwa kadi ya njano baada ya kujiagusha ndani ya 18 na
kujindai kuwa kaangusha hadi mapumziko wenyeji walikuwa mbele kwa goli
hilo moja.
Kipindi cha pili kilianza kwa wenyeji
kuanza kulishambulia lango la Stars na mnomo dakika ya 54,Mathew Rusike
alifunga bonge la goli kwa shuti baada ya Musona kuukosa mpira na
kumkuta mfungaji akiwa na nafasi ya goli na kumchungulia Aisha Manula na
kumuacha akiwa hana la kufanya.
Alikuwa Musona tena dakika ya 56 alifunga goli la tatu kwa kichwa baada ya kupokea mpira toka kwa Willard Katsande
ikumbukwe kuwa Knowledge Musona anacheza Ligi moja na Samatta na katika
klabu yake ya KV Oostende anaongoza kwa ufungaji akiwa na magoli sita
na timu yake inashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 25 na msimamo wa
wafungaji anashika nafasi ya nne.
Hadi mwamuzi anapuliza kipyenga cha
mwisho Warriors wameibuka na ushindi wa jumla ya magoli 3-0 na kwa
matokeo hayo yamewapa faida Wazimbabwe kuelekea katika viwango vya
FIFA,kwa sasa Zimbabwe wapo nafasi ya 110 katika ubora wa viwango vya
FIFA na Tanzania wamashika nafasi ya 144 na kwa kufungwa kwao
kutawafanya washuke chini zaidi wakati orodha itakapotolewa na FIFA.
0 comments :
Post a Comment