Chadema Yataka Mkapa Anyang'anywe Shamba Kwa Kutoliendeleza Kama Sumaye

Meya wa Manispaa ya Ubungo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA), Boniface Jacob amemtaka Rais Dk Magufuli kulichukuwa shamba linalomilikiwa na Rais Mstafuu Mzee Benjamin Mkapa kama alivyofanya kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.

Meya huyo alisema kuwa kiongozi huyo wa zamani na familia yake wanamiliki shamba kubwa katika wilaya ya Ubungo ambalo halijaendelezwa kwa muda mrefu sasa.

Meya huyo ambaye amekuwa Diwani wa Ubungo kwa muda mrefu ametaa shamba hilo lililopo Mbezi, Dar es Salaam lirejeshwe kwenye halmashauri ili liweze kufanyiwa shughuli nyingine.

Hoja hiyo ya Meya wa Kinondoni imekuja siku chache tangu aliyekuwa Waziri Mkuu katika serikali ya awamu ya tatu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Frederick Sumaye aliponyang’anywa shamba lake eneo la Mabwepande ambalo hajaliendeleza kwa muda.

Meya alitoa maelezo hayo alipokuwa akizungumza na gazeti la mwananchi ambapo alisema kuwa watamuandikia Rais Magufuli barua wakimuomba abatilishe umiliki wa shamba hilo aipe Manispaa ya Ubungo ambayo ndiyo kwanza imeanzishwa
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment