MZEE Athuman Mchambua (76), ambaye ameweka tangazo nyumbani kwake la kutafuta mke, ameongeza sharti jipya kwa mke anayemuhitaji.
Amesema licha ya kupokea simu nyingi kutoka maeneo mbalimbali nchini, lakini amewataka wanawake ambao atawafanyia usaili, hasa kwa yule ambaye atakuwa ameshinda, kutobweteka kwani atakuwa katika kipindi cha mpito cha ndoa yake.
Mzee huyo amelieleza gazeti la Mtanzania kuwa amefikia hatua hiyo ili kuanza kupitia majina ya wanawake zaidi ya 30 ambao tayari wamejaribu bahati ya kuolewa naye.
Alisema kuwa haoni haja tena ya kuendelea kuweka tangazo hilo kwa kuwa asilimia kubwa ya wanawake wanaojitokeza hushindwa kukidhi vigezo anavyovihitaji.
Alivitaja vigezo sita muhimu vya mwanamke anayemuhitaji kuwa ni awe mcha Mungu na mwenye kutunza watoto wake.
“Vigezo vingine awe na sifa ya ndoa, awe na sifa ya mume, awe na sifa ya kilimo, awe na sifa ya kutunza watoto na awe na sifa ya usafi wa hali ya juu.
“Tangu kuanza nimepata wanawake zaidi ya 30 ambao wanne kati yao wamefika hapa nyumbani kwangu, lakini wengine wamekuwa wakiona aibu kuja hapa moja kwa moja na hivyo wamekuwa wakitumia simu. Leo (jana) nimewafanyia usaili wanawake watano kwa simu, lakini hakuna hata aliyefuzu nusu ya vigezo, wengi wamekuwa wakiteleza sifa ya kilimo,” alisema
0 comments :
Post a Comment