Na.Alex Mathias.
Bao la kiungo mkabaji wa zamani wa Yanga,Frank Domayo
dakika ya 33 limeipeleka Azam FC Fainali ya Michuano ya kombe la
Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar kwenye uwanja wa Amaan.
Frank Domayo aliachia shuti la
mita 18 na kumuacha mlinda mlango wa Taifa Jang’ombe akiwa hana la
kufanya na kupelekea timu hizo kwenda mapumziko Azam Fc wakiwa
wanaongoza kwa bao hilo.
Kipindi cha pili kilianza kwa
Taifa Jang’ombe kulishambulia lango la Azam kama nyuki huku wakikosa
nafasi nyingi wakati Matajiri wa jiji la Dar es salam wakicheza kwa
mashambulizi ya kushtukiza huku wakilinda bao lao.
Baada ya kuona kosakosa nyingi
timu zote zilifanya mabadiliko mbalimbali hata hivyo mabadiliko hayo
hayakuwasaidia Jang’ombe na kukubali kipigo toka kwa Azam ambao
wametinga Fainali itakayochezwa siku ya Ijumaa ya Januari 13,2017.
Kwa Matokeo hayo Azam wanasubiri
mshindi kati ya mahasimu wa kariakoo Simba na Yanga ambao wanatarajia
kumenyana majira ya saa 2:15 kwenye uwanja huo huo wa Amaan.
Ngoja tusubiri ni Simba au Yanga
atakwenda kucheza na Azam FC Fainali ya 11 ya Kombe la Mapinduzi ya
mwaka 2017 ambapo tayari bingwa mtetezi alishavuliwa ubingwa na timu ya
Taifa ya Jang’ombe.
0 comments :
Post a Comment