Askari wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za
Afrika Magharibi (Ecowas) wamegundua kemikali ya sumu kali iliyokuwa
imetegwa kwenye vyumba vya Ikulu.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Ecowas kupitia gazeti la Freedom la Gambia, kemikali hiyo ilitegwa kwa lengo la kuua mtu yeyote atakayeingia ndani ya Ikulu hiyo.
Kutokana na hali hiyo, kiongozi mpya wa Gambia, Adama Barrow anatakiwa kuendelea kukaa Senegal kwa usalama wake huku uchunguzi ukiendelea kufanyika.
0 comments :
Post a Comment