Kocha
wa Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa timu yake kwa sasa
inaweza kuondoka katika zile timu zinazowania ubingwa baada ya kupokea
kichapo cha 4-0 kutoka kwa Everton.
Kwa sasa City wapo nyuma kwa alama
10 dhidi ya vinara Chelsea wenye alama 52 na alipoulizwa kama alama 10
ni nyingi sana alijibu ndio sio rahisi kuzifikia.
Guardiola, mwenye miaka 45,
amewaambia wachezaji wake kuungana wakati huu wa kipindi kigumu na
kutoangalia msimamo wa ligi mpaka mwisho wa msimu.
”Mwishoni mwa msimu tutajitathimini kiwango chetu,ufundishaji ulikuwaje na wachezaji walikuwaje.
Baada ya hapo tutaamua kwa pamoja
kocha huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich amesema kuwa ana
furaha sana kuwa ndani ya Manchester licha ya timu yake kuwa nafasi ya
tano.


0 comments :
Post a Comment