Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mhandisi Lili-Ang kutoka
kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) inayakarabati
na kujenga uwanja wa ndege wa Mwanza.
Mhandisi Mshauri anayesimamia ukarabati na
ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza akimuonesha Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa Mnara wa jengo la
kuongozea ndege alipokagua ujenzi wa uwanja huo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa viongozi wa uwanja wa ndege
wa Mwanza namna ya kushirikiana na Mkandarasi Beijing Construction
Engineering Group (BCEG) anayekarabati na kujenga uwanja huo.
Muonekano wa jengo jipya la kuongozea
ndege linalojengwa na kampuni ya Beijing Construction Engineering Group
(BCEG) katika uwanja wa ndege wa Mwanza.
…………
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa amemtaka Mkandarasi anayejenga na kukarabati
uwanja wa ndege wa Mwanza Beijing Construction Engineering Group (BCEG),
kuhakikisha ujenzi huo unakamilika ifikapo Novemba mwaka huu.
Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi
wa mnara wa kuongozea ndege, jengo la kuhifadhia mizigo, eneo la
kuegeshea ndege na jengo la umeme litakalotoa huduma katika uwanja huo,
Profesa Mbarawa amesema tayari Serikali imeshamlipa mkandarasi huyo
kiasi cha shilingi bilioni saba kwa ajili ya ujenzi huo.
“Sisi tumeshamlipa pesa yake yote na hivyo
tunachotaka kwake ni kukakamilisha kazi yetu kwa wakati ili kuupa hadhi
inayostahili uwanja wa ndege wa Mwanza amboa ni kiungo muhimu katika
kanda ya Ziwa”, Amesema Profesa Mbarawa.
Prof. Mbarawa amemuagiza Meneja wa uwanja
wa ndege wa Mwanza Bi .Easter Madale kuhakikisha vikwazo vyote
vinavyomkabili mkandarasi vinaondolewa ili kumuwezesha kufanya kazi
kubwa kabla ya kipindi cha mvua za masika zinazotarajiwa kuanza mwezi
machi.
Kwa upande wake Mhandisi Lili Ang
aneyesimamia ujenzi huo kutoka kampuni ya BCEG amemhakikishia Prof.
Mbarawa kuwa baada ya kupokea malipo wamejipanga kukamilisha kazi hiyo
kwa wakati na viwango ili waweze kupata fursa nyingine za ujenzi hapa
nchini.
Naye Meneja wa Uwanja wa ndege wa Mwanza
Bi .Easter Madale ameyataka mashirika ya ndege kuongeza safari za ndege
kwenye uwanja wa Mwanza kwa kuwa sasa utakuwa na hadhi ya kimataifa na
kusisitiza umuhimu wa wawekezaji wa hoteli, vituo vya mafuta na maduka
makubwa kuwekeza karibu na uwanja huo ambao ndio lango la uchumi wa
kanda ya ziwa.
Katika hatua nyingine Waziri wa
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano ameelekea mkoani Simiyu kuanza ziara ya
siku mbili mkoani humo amabapo pamoja na mambo mengine anatarajiwa
kushiriki katika ufunguzi wa barabara ya Bariadi- Lamadi iliyojengwa kwa
kiwango cha lami.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawssiliano


0 comments :
Post a Comment