Mbunge
wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde amesema kitendo alichofanya Mbunge
mwenzake wa Jimbo la Mara CCM, Boniface Getere cha kugawana muda na
mbunge wa Serengeti (Chadema), Marwa Ryoba ni utovu mkubwa wa nidhamu.
Lusinde
ni mmoja wa wabunge wa CCM waliomlalamikia Getere kumpa dakika tano
Ryoba ili aweze kuchangia taarifa za kamati za Bunge Kamati ya Ardhi,
Maliasili na Utalii na ya Kilimo, Mifugo na Maji baada ya mwenyekiti wa
Bunge, Mussa Hassan Zungu kumruhusu azungumze kwa dakika kumi.
“Duniani
kote kazi ya upinzani ni kuipinga Serikali iliyopo madarakani na kazi
ya wabunge wa chama tawala ni kuishauri Serikali na kuipongeza pale
inapofanya vizuri, hizi ni kambi mbili tofauti,huwezi kuwapa muda
wapinzani” alisema Lusinde.
Mbunge
wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea alisema haoni ubaya kwa mbunge wa CCM
kumpa muda mbunge wa upinzani bali anachokiona CCM wanahamishia kampeni
bungeni.
Hata
hivyo, alipoulizwa Getere iwapo haoni kama amefanya makosa kumgawia
mbunge wa upinzani, alisema hajaona madhara yoyote kwa kitendo chake
hicho.
0 comments :
Post a Comment