Wakati Yanga ikikwea pipa kesho kwenda Comoro kuikabili timu ya Ngaya
Club de Mbe katika mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika, watani
zao Simba watakuwa kwenye dimba la Taifa jijini hapa kusaka poiti tatu.
Simba ina pointi 48 ikiwa nyuma ya Yanga kwa pointi moja na Yanga na
ushindi wowote itakaoupata kwenye dimba hilo dhidi ya Prisons ya Mbeya
itakuwa na maana kwamba inarejea kwenye usukani wa ligi.
Rekodi zinaonyesha kuwa katika michezo mitano ya karibuni baina ya Simba
na Prisons, Wekundu wa Msimbazi wameshinda miwili wakati maafande hao
wakishinda miwili huku mchezo mmoja timu hizo zikitoka sare.
Utamu wa mechi hiyo ni ushindani uliopo baina ya mabeki wa Simba chini
ya mkongwe Method Mwanjali na Novaty Lufunga dhidi ya washambuliaji
Prisons, Victor Hangay na Lambart Subiyanka.
Kocha wa msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja ametambia ushindi walioupata
dhidi ya Majimaji ya Songea katika mchezo uliopita wa mabao 3-0 kuwa
umewaongezea ari ya kuiua Prisons.
Naye Kocha wa Prisons, Abdallah Mohammed amesisitiza kwamba licha ya mchezo kuwa mgumu, lakini ushindi ndiyo matarajio yao.
0 comments :
Post a Comment