Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Aikael Mbowe (MB) leo tarehe 10
February 2017 amefungua kesi ya kikatiba dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salam, Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu DSM na Kamanda wa Polisi wa
Kanda Maalumu Dsm.
Kesi hiyo ilisajiliwa kama Kesi ya Kikatiba namba 1 ya 2017 imefunguliwa
kwenye Mahakama ya Kuu masijala ya Katiba (Masijala Mkuu).
Kwenye Kesi hiyo Mbowe anaomba Mahakama Kuu itamke na kuwa Mkuu wa Mkoa hana mmalaka ya kudharilisha, na kukamata.
Mbowe pia ameiomba mahakama itengue vifungu vya 5&7 vya Sheria ya
Tawala za Mitaa kwakua ni batili na vinakiuka haki za kikatiba.
Katika kesi hizo Mbowe atawakilishwa na Mawakili toka Kurugenzi ya Katiba Sheria na Haki za Binadamu ya CHADEMA.
0 comments :
Post a Comment