Mtandao
wa TUKO umeripoti kuhusu huyu Mwanamke aliyewaaacha wengi na mshangao
baada ya kutumia njia isiyo ya kawaida kumzuia mumewe kuchepuka na
kuchukua Mwanamke mwingine.
Mwanamke
huyo Mkenya aliyetambulika kwa jina la Wanjiru Kamami ama Shiro
alichapisha tangazo kwenye gazeti moja la Kenya akitaka kujuzwa habari
na yeyote atakayemwona mumewe akiwa na ‘mpango wa kando’ au Mchepuko.
Katika
kitendo cha Mwanamke huyo kuonyesha kwamba yuko serious akaamua
kuandika na jina la mume wake pamoja na namba ya simu kwenye hilo
tangazo lililosomeka "Hii ni kuwajulisha kwamba huyu aliye kwenye picha ni Mume wa Wanjiru Kamami toka mwaka 1982
"Ukimuona
anadanganya Wasichana wa shule, Wanawake wengine au kina mama wa
sokoni, mwambie aende nyumbani kwa mke wake au piga simu au sms kwenye
0751 993 571"
0 comments :
Post a Comment