Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar es
Salaam, Anthony Lusekelo 'Mzee wa Upako' amefunguka na kuweka wazi kuwa
yeye anapenda sana magari na katika magari hayo yeye anapendelea zaidi
magari makubwa makubwa.
Akiongea kwenye kipindi cha KIKAANGONI , Mzee wa Upako alisema kuwa
hapendi kabisa "vigari vidogo vidogo" na kudai kuna gari hawezi kabisa
kuendesha.
"Mimi napenda sana magari mazuri mazuri kwa sasa natumia gari aina ya V8
Land Cruiser ile kubwa kabisa. Napenda gari kubwa Benz, BMW, Land
Cruiser zile kubwa kabisa hizi ndiyo gari nazopenda sana kwa hiyo hizo
zingine inategemea naweza kuendesha maana wakati mwingine unaangalia na
hali kama hali ikiwa mbaya basi unatembelea hata bajaji ila mimi napenda
magari makubwa" alisisitiza Mzee wa Upako
Pia hakusita kutaja aina ya gari ambayo hawezi kuendesha kuwa ni Vits
"Kuendesha Vits hata siku moja siwezi, hivi vigari vidogo vidogo hivi
hapana sitaki, yaani sipendi"



0 comments :
Post a Comment