Simba :Hatutacheza Na Watani Zetu Yanga Kwa Waamuzi Wa Ndani Ya Nchi

Image result for HAJI MANARA 
Uongozi wa klabu ya simba umesema hautacheza mchezo wowote wa ligi dhidi ya watani wao wa jadi Yanga endapo waamuzi hawatatoka nje ya nchi tena wenye uzoefu wa mechi kubwa wanaotambuliwa na Fifa. 

Simba wapo tayari kulipa gharama za waamuzi hao kuanzia mwamuzi wa kati na wasaidizi wake wawili ili haki itendeke kwakua watani wao wamekuwa wakipendelewa mara kwa mara na marefarii wa hapa nchini. 

Msimamo huo umetolewa na msemaji wa klabu hiyo Haji Manara alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari klabuni hapo na kusema kuwa kwasasa hawatakuwa tayari kuona haki zao zikidhulumiwa kwa namna yoyote na wataanzia mzunguko wa pili unaotarajia kuanza Disemba 17.

"Kila mtu aliona jinsi mwamuzi Jonensia Rukyaa alivyotunyonya msimu uliopita na Matrin Saanya mechi iliyopita sasa hatutaki muamuzi yoyote wa Tanzania kwenye mechi dhidi ya Yanga. Mechi ya Zamalek na Al Ahly waamuzi wanatoka nje ya Misri na sisi tunataka hivyo " alisema Manara. 

Wakati huo Manara ameishangaa kamati ya masaa 72 ya shirikisho la mpila wa miguu nchini TFF kuendelea kufanya Uchunguzi juu ya sakata la Samuel Mpenzu wakati mengine tayari wametoa maamuzi na adhabu pia. 

" Tangu mchezo watu na Yanga hadi leo ni siku 53 zimepita lakini bado Uchunguzi unaendelea, makocha wa Azam na Yanga timu pamoja na wachezaji waliofanya makosa mzunguko wa kwanza wamepata Adhabu kwanini suala la Saanya hadi leo linasubiri Uchunguzi ? "alihoji Manara. 

CREDIT TO :SOKA EXTRA
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment