Maafisa wa UN na raia wanne wa DRC walitekwa nyara na kupelekwa katika msitu.
Maafisa wawili wa Umoja wa Mataifa wametekwa nyara katika jimbo la
Kasai ya Kati, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, chanzo cha
usalama katika umoja wa mataifa kimebaini
Mateka hao ni Michael Sharp kutoka Marekani na Zaida Kikatalani, raia wa Sweden.
Kwa mujibu wa serikali ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo, watu hao pamoja na raia wanne wa DRC (waendesha
pikipiki za kukodiwa na mkalimani wao) walitekwa nyara na kupelekwa
katika msitu.
Mkoa wa Kasai ya kati, wakumbwa na uasi
Vurugu baina ya vikosi vya usalama na wanamgambo zimeendelea kuukumba mkoa wa Kasai ya Kati tangu mwezi Septemba 2016.
Makabiliano hayo tayari yameingia katika mkoa jirani wa Kasai Mashariki na Lomani.
Karibu watu mia nne wameuawa katika machafuko hayo yanayoendelea katika maeneo hayo.RFI
0 comments :
Post a Comment