Bahati mbaya msimu huu sio mzuri kwa Man United kwani wamejikuta wakiambulia kupoteza mchezo wa robo fainali ya FA kwa kufungwa kwa goli 1-o, goli la Chelsea lilifungwa dakika ya 51 na N’golo Kante akipiga shuti nje ya 18 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Willian.
Kipigo hicho kinakuwa ni kipigo cha 52 cha Man United kuwahi kufungwa na Chelsea katika jumla ya michezo 176 yao waliyowahi kukutana, huku Man United akiifunga Chelsea mara 75 na sare mara 49, mara ya mwisho Man United kupata matokeo dhidi ya Chelsea Stamford Bridge ilikuwa October 28 2012.
0 comments :
Post a Comment