WAKATI Yanga ikishuka Uwanja wa Taifa leo kuivaa Ruvu Shooting ya Pwani
katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, beki wa kati wa kimataifa Togo,
Vincent Bossou, amesema yuko tayari kuondoka katika klabu hiyo, lakini
baada ya kulipwa malimbikizo ya mishahara yake ya miezi minne anayoidai
klabu hiyo.
Bossou aliandika madai yake jana katika akaunti yake ya Instagram na
kukanusha taarifa kuwa anadai mshahara wa mwezi mmoja tu wa Januari kama
uongozi wa timu hiyo ulivyoeleza.
Beki huyo alisema yeye ni mchezaji na ili aweze kufanya kazi yake
vizuri, ni vyema uongozi ukatimiza mahitaji yake ambayo walikubaliana.
"Waambie (viongozi) wanilipe mshahara wangu wa miezi minne, ni rahisi
nitaondoka, (***’tusi’)," aliandika beki huyo wa timu ya Taifa ya Togo
akiwajibu mashabiki wa wanaodaiwa kuwa wa Yanga ambao wanamtaka aondoke
kwenye timu yao.
Mtogo huyo, tayari ameshaonyesha mipango yake ya kuachana na mabingwa
hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kugoma kusaini mkataba
mpya mapema mwaka huu kama alivyotakiwa na uongozi.
Nyota wengine ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu na
wamekaa mguu ndani mguu nje ni pamoja na mshambuliaji wa kimataifa
kutoka Zimbabwe, Donald Ngoma na winga Simon Msuva.
0 comments :
Post a Comment