Video:Msimamo Wa Jukwaa La Wahariri Kwa CUF Ya Lipumba Baada Yakushambulia Waandishi Wa Habari

Jukwaa la Wahariri Tanzania ‘TEF’ leo April 26, 2017 limekutana na waandishi wa habari kuzungumzia tukio la kushambuliwa kwa waandishi wa habari wakati wanatekeleza wajibu wao kitaaluma Jumamosi April 22, 2017.
Katika tukio hilo waandishi wa habari walishambuliwa na wafuasi wa CUF upande wa Prof. Ibrahim Lipumba ambapo kutokana na kitendo hiko, TEF wametoa msimamo wao ikiwa ni pamoja na kumtaka Prof. Lipumba kutoa kauli binafsi kama alivyofanya Maalim Seif aliyeandika barua kwa TEF akilaani kupigwa kwa wanahabari hao na kutoa pole.
Akieleza kusikitishwa kwake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Theophil Makunga amesema: “Jukwaa la Wahariri Tanzania limeshtushwa kushambuliwa na kuumizwa kwa waandishi wa habari ambao walikuwa wakitekeleza wajibu wao kitaaluma mwishoni mwa wiki iliyopita.” – Theophil Makunga.
Bonyeza play kutazama…

VIDEO: “Hatuna sababu ya kukataa, sisi tulituma vijana wetu”- CUF. Bonyeza play kutazama…
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment