Diwani Chadema Kitwiru -Iringa Apewa Masaa Kuomba Msamaha Na Mkuu wa Wilaya Iringa Mjini



DIWANI wa Kata ya Kitwiru, Manispaa ya Iringa, Baraka Kimata (Chadema), amechafua hali ya hewa wakati wa kupokea Mwenge wa Uhuru kwa kusema kuwa ikiwa chama chake kitachukua nchi, watauhifadhi mwenge huo Makumbusho ya Taifa.

Kauli hiyo aliitoa jana alipopewa nafasi ya kusalimia wananchi katika viwanja vya Mlandege wakati wa kupokea mwenge huo uliokuwa ukiendelea na mbio jana wilayani hapa.

Kutokana na kauli hiyo, baadhi ya wananchi walipigwa na butwaa, huku kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa, Amour Hamad Amour, akimwaga chozi hadharani kutokana na kauli ya diwani huyo.

Akizungumza na wananchi kuhusu kauli ya diwani huyo, Amour alisema kuwa kipindi hiki si cha siasa ila Watanzania wanapaswa kufanya kazi pamoja.

 “Tumeumia sana sisi kama wakimbiza mwenge kitaifa, hata nyinyi nyuso zenu zinaonyesha huzuni, hiki si kipindi cha siasa, tunapaswa kutenganisha siasa na mambo ya kitaifa, tunapaswa kuonyesha uzalendo kwa nchi yetu na wala sio kupotosha umma wa Watanzania juu ya Mwenge wa Uhuru,” alisema Amour.

Baada ya maelezo hayo, alisimama Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela na kutoa saa 26 kwa diwani huyo kuandika barua ya kuomba radhi, ikiwamo kueleza kwanini alitaka kusababisha vurugu wakati ujumbe wa Mwenge wa Uhuru ukielekea katika uzinduzi wa miradi ya maendeleo.

Alimtaka Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) Iringa, kuhakikisha diwani huyo anafikisha barua hiyo ofisini kwake na ikiwa atakiuka agizo hilo, hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment