TAARIFA ZA AWALI
Masaa kadhaa baada ya kuiongoza timu yake ya Simba SC kurejea katika anga ya kimataifa kwa ushindi wa kombe la Azam Sports Federation Cup dhidi ya Mbao FC, kiungo wa Simba Jonas Mkude ameripotiwa kupata ajali mbaya akiwa njiani kurejea Dar es Salaam akitokea Dodoma.
Nahodha huyo wa Simba amepata ajali hiyo maeneo ya Mitibora, Dumila mkoani Morogoro akiwa njiani kurejea Dar es Salaam kuiwahi Taifa Stars. Taarifa za awali zinasema ameumia maeneo ya shingoni, amekimbizwa kwenye hospitali ya mkoa wa Morogoro pamoja na majeruhi wenzie ambao baadhi wana halimbaya.
Kwenye gari ambayo Mkude amepata nayo ajali walikuwepo watu 6, na kilichopelekea ajali hiyo ni kupasuka kwa tairi la nyuma. Majeruhi mmoja yuko mahututi.
UPDATE KAMILI
Gari walilokuwa wakisafiria baadhi ya wachezaji na mashabiki wa klabu ya Simba akiwemo nahodha wa kalabu hiyo Jonas Mkude limepinduka maeneo ya Dumila mkoani Morogoro
baada ya tairi ya gari ya nyuma kupasuka.
walipokuwa njiani kutokea Dodoma
Shabiki mmoja mwanamke aliyejulikana kwa jina la Shose amefariki baada ya kupata majeraha makubwa. Jonas Mkude alipata majeraha madogo sana na yupo salama, majeruhi wengine wawili waliokuwemo kwenye gari hiyo wamewahishwa kwenye hospital ya Morogoro.
Jonas mkude na wachezaji wengine waliokiwa kwenye gari lingine walikuwa wanaiwahi kambi ya timu ya Taifa.
Klabu ya Simba inatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki no wapenzi wote wa klabu ya Simba.
Klabu ya Simba inaendelea kuwasiliana na ndugu wa marehemu kwa ajili ya kushirikiana katika msiba mzito kwa klabu nzima ya Simba kwa kumpoteza Shabiki wake mkubwa ambaye alikuja Dodoma kuisapoti timu yake pendwa ya Simba katika kuchukua ubingwa.Facebook