HUSSEIN Bashe, Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini, mkoani Tabora ameitaka Serikali kutoa kauli juu ya Sh. 200 milioni ambazo Disemba 2016, Rais John Magufuli aliahidi kuzitoa kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya maji katika jimbo hilo,
Bashe ameliambia Bunge kuwa Disemba mwaka jana, Rais Magufuli alitoa ahadi ya Sh. 400 milioni kwa ajili ya kutatua tatizo la maji, Nzega Mjini lakini mpaka sasa ametoa Sh. 200 milioni tu na kumtaka Isack Kamwelwe, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji kueleza ni lini fedha zilizobaki zitatolewa.
“Tulipokea milioni 200 tu, Mhe. Naibu Waziri unawaambia nini Wananchi wa mji wa Nzega juu ya utekelezaji wa fedha iliyobaki ambayo tumekuwa tukisubiri tangu Aprili mwaka huu?” alihoji Bashe.
Ambapo naibu waziri Kamwelwe alijibu akisema, “Ni kweli Rais alitoa ahadi ya kupeleka milioni 400 kwa ajili ya kuboresha huduma ya maji katika Mji wa Nzega. Milioni 200 tumeshaikabidhi Mamlaka ya Maji ya Tabora na tutapeleka fedha zilizobaki siku za hivi karibuni.
Kamwelwe alisema kupitia mradi mkubwa wa maji wa kutoka Solwa kwenda Nzega na Tabora uliosainiwa hivi karibuni miundombinu itakarabatiwa.
Kwa upande wake John Mnyika Mbunge wa Kibamba, swali lake liliulizwa na Mbunge wa Vunjo, James Mbatia ambapo lilihoji;
“Jimbo la Kibamba linapaswa kuhudumiwa kwa sehemu kubwa na maji ya kutoka mtambo wa Ruvu Juu, je ni kwanini miradi ya maji imechelewa kukamilika kinyume na ratiba inayotolewa na Serikali?” alihoji na kujibiwa;
“Maeneo yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu Juu ni pamoja na Mlandizi, Visiga, Picha ya Ndege, Tumbi na Pangani.
“Maeneo haya yataanza kupata maji baada ya kukamilika kwa mradi wa mfumo wa kusambaza maji ambao unaendelea kutekelezwa na kampuni ya Jain Irrigation System Ltd.”
0 comments :
Post a Comment