Manara, amezidi kuwatia hofu wapenzi na mashabiki wa Yanga kuhusu usajili wa Haruna Niyonzima
Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara, amezidi kuwatia hofu wapenzi na mashabiki wa Yanga kuhusu usajili wa Haruna Niyonzima.
Kupitia akaunti yake ya instagram, msemaji huyo wa Simba ameweka picha yake akiwa na kiungo mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima ambaye mkataba wake umemalizika tangu msimu uliomalizika
“Mwana kulitaka ,mwana kulipawa, Napita zangu washikaji”alimalizia kwa ujembe huo Manara
Kutokana na posti hiyo aliyoiweka Haji Manara imezua mjadala mkubwa kwa mashabiki wa Simba na Yanga kuhusu usajili wa Haruna Niyonzima
Ila kwa habari ambazo bado siyo rasmi ni kwamba klabu ya Yanga tayari imeshamalizana na Niyonzima, na Mnyarwanda huyo amesaini kandarasi ya miaka miwili kukipiga JangwaniFacebook