Akimwakilisha Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu kwenye ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa maswala ya kijinsia ulioandaliwa na Chuo Cha Ualimu (DUCE), WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alisema,
“Tunapokataza watoto wa kike wasiendelee na masomo pindi wanapopata ujauzito wakiwa mashuleni tunawaadhibu watoto wa masikini washindwe kutimiza malengo yao kwa wakati waliotarajia”
Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kasema, kwenye utawala wake hakuna mwanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi sekondari atakayepata mimba au mtoto atakayerudi darasani.
0 comments :
Post a Comment