Pwani. Rais John Magufuli amemwagiza Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, kuwanyang’anya viwanda wamiliki ambao wameshindwa kuviendeleza.
Ameyazungumza hayo leo (Alhamisi) akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani ambako amezindua viwanda saba.
“Kipindi cha nyuma tulipofanya makosa ni pale tulipouza viwanda kwa watu binafsi, sasa kuna viwanda 197 vimeshakufa waliouziwa hawajishughulishi na vingine vipo kama magofu,” amesema.
Kutokana na hilo, Rais amesema; “natoa wito kwa wote waliouziwa viwanda kipindi cha nyuma na sasa wameshindwa kuviendeleza , naagiza sasa basi mrudishe na wewe Waziri Mwijage tumia hata
nguvu kama kuwaweka ndani weka tu siku akitoka huko atakuta kiwanda kimeanza kazi.”