Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amekamatwa na polisi wanne na kupelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo, amezungumza na wanahabari leo saa 12 jioni na kueleza kuwa Mdee amekamatwa akiwa nyumbani kwake Makongo Juu.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo, amezungumza na wanahabari leo saa 12 jioni na kueleza kuwa Mdee amekamatwa akiwa nyumbani kwake Makongo Juu.
Awali akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi aliagiza Jeshi la Polisi kumkamata mbunge huyo kwa madai kuwa amemkashifu Rais John Magufuli.
Kamanda wa Polisi, mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda amesema amefanya hivyo kwa amri ya mkuu huyo wa wilaya.
0 comments :
Post a Comment