Afisa misitu asimamishwa kazi kwa tuhuma za kufuja milioni mia tisa

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mjini limemsimamisha kazi Afisa Misitu wa Wilaya hiyo David Hyera kwa tuhuma za kufuja pesa zaidi ya milioni mia tisa zilizotokana na uvunaji wa miti katika msitu wa Mbambi.
Kwa mujibu wa maelezo ya Afisa Misitu wa Halmashauri ya Mbinga Mji Mkoani Ruvuma, David Hyera, ambaye ndiye anayetuhumiwa kuingizia hasara halmashauri hiyo amesema katika Hekari 75 za Msitu wa Mbambi kulikuwa na miti elfu tano mia nne na robaini na nne ambapo kila mti ulitoa mbao 10 na pesa iliyopatikana ni milioni 195, Jambo ambalo madiwani hawakubaliani nalo.
Madiwani hao wameazimia kusimamishwa kazi Afisa misitu wa halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji pamoja na kuundwa kwa tume mbili za uchunguzi moja ikiwa ni ya halmashauri na ya pili inaundwa na mkuu wa wilaya hiyo
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment