Mkuu wa wilaya ya ilala jijini Dar es Salaam Bi.Sophia Mjema amepiga marufuku vijana wa ulinzi shirikishi kujishughulisha na ukamataji wa bodaboda badala yake vijana hao wasaidie kufichua wizi na vitendo vingine vya kihalifu ili jeshi la polisi liweze kuchukua hatua Mkuu huyo wa wilaya ya ilala ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na madereva bodaboda kutoka katika wilaya hiyo baada ya kupokea maandamano ya amani yaliyofanywa na madereva hao
kwa lengo la kumpongeza Rais Mh. John Pombe Magufuli kwa hatua mbali mbali anazozichukua katika
kukabiliana na vitendo vya rushwa na ubadhilifu wa mali za Umma.
kukabiliana na vitendo vya rushwa na ubadhilifu wa mali za Umma.
Madereva hao wametumia fursa hiyo pia kuwasilisha kero mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kuruhusiwa kuingia katikati ya jiji huku kamanda wa polisi kikosi cha usalama barabarani mkoa wa kipolisi wa ilala Peter Mashishanga akizijibu na kuwataka madereva hao kutoa taarifa za wao kuombwa rushwa na polisi wa usalama barabarani ili aweze kuchukua hatua
0 comments :
Post a Comment