Afungwa jela maisha kwa kubaka na kumlawiti mtoto wa miaka 8


Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kilimanjaro imetoa hukumu ya kesi iliyokuwa ikimkabili ndg Benedict Joachim Kimario (46) ambaye ni mzaliwa wa Kijiji cha Mrao Kata ya Mraokeryo iliyopo Tarafa ya Mashati wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, ambapo alikuwa akituhumiwa kwa kumbaka na kumlawiti mtoto Lucia Faustini Kitalala (08) ambae ni mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Mkovanda wilayani humo.
Akisoma hukumu hiyo mbele ya mahakama ya hakimu mkazi mkoani humo, hakimu Aidadi Hendry Mwilapwa amesema kuwa mtuhumiwa atakwenda kutumikia kifungo cha maisha jela kwa kutenda makosa mawili tofauti ambayo ni ubakaji na kosa la kulawiti. Makosa hayo kila moja limetolewa hukumu yake kulingana na sheria za nchi ambapo kulingana na uzito wa makosa hayo mahakama imetoa hukumu ya kifungo cha maisha kwa mtuhumiwa huyo ambaye pia ni mfanyabiashara wa madini wilayani Mererani mkoani Arusha.
Inaelezwa kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo tarehe 10/05/2016 ambapo alimbaka na kumlawiti mtoto huyo na kisha kukimbilia Mererani kabla ya kutiwa nguvuni na jeshi la polisi wakishirikiana na Diwani wa Kata ya Mraokeryo, Athuman Kimario.
Akizungumza baada ya hukumu hiyo mapema leo Diwani wa Kata ya Mraokeryo, Athuman Kimario, amesema kuwa kesi hii imechukua muda mrefu lakini anaishukuru mahakama kwa kutenda haki.
“Kesi hii imechukua muda mrefu kwa kweli lakini leo hii mahakama imetenda haki na hii itakuwa fundisho hasa kipindi hiki ambacho matukio ya ubakaji na ulawiti yanazidi kupamba moto katika kata yangu”
Amesema diwani huyo na kuongeza kuwa atahakikisha kuwa mtu yeyote atakaejihusisha na vitendo vya
ubakaji na ulawiti katika kata yake anaripotiwa kwa vyombo husika ili hatua kali zichukuliwe dhidi yake na hatimae iwe ni mwarubaini wa tatizo hilo kwenye kata yake.
Aidha, wazazi wa mtoto Lucia mbali na kuishukuru mahakama kwa kutenda haki, wamempongeza diwani huyo na kumtaka aendelee na uwajibikaji na weledi aliouonesha kwenye kesi dhidi ya mtoto wao.
Hukumu ya mshtakiwa Benedict imekuja wakati ambao mkazi mwingine wa kata hiyo anayefahamika kwa majina ya Amedeus Clemens akishikiliwa na jeshi la polisi kufuatia kutuhumiwa kumbaka na kumlawiti mtoto wa miaka minne ambae naye ni mkazi wa kata hiyo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment