Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro limewafukuza kazi watumishi wake watatu akiwemo Afisa Nyuki Mwandamizi Mbaraka Barazae kwa tuhuma za utoro kazini huku maafisa watendaji wawili wakifukuzwa kwa tuhuma za kumuibia mwajiri wao zaidi ya shilingi milioni 52.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo David Ligazio amesema watumishi hao wametenda makosa hayo kinyume na kanuni namba 51 na 52 za utumishi wa umma za mwaka 2003 na kutaka watumishi wengine kubadilika na kuacha kufanya kazi kwa mazoea
0 comments :
Post a Comment