CHADEMA Kutoa Tamko Zito Leo

Mwenyekiti  wa Chama  Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, leo  anatarajiwa kutoa maazimio mazito ya Kamati Kuu ya  chama hicho iliyokutana kwa siku mbili, Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa   Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema, ilisema pamoja na mambo mengine, kamati hiyo ilijadili kwa kina hoja tatu za msingi.

Alitaja hoja hizo kuwa ni hali ya mwenendo wa  siasa na ukandamizaji wa demokrasia, kuporomoka kwa uchumi na hali ngumu ya maisha inayowakabili Watanzania.

Alisema  hoja ya tatu ni kamatakamata inayoendelea kufanywa na vyombo vya dola  dhidi ya viongozi, wanachama na wafuasi  wa chama hicho katika maeneo mbalimbali.

“Pamoja na  mambo niliyotaja hapo juu, tunategemea mwenyekiti wetu atatoa maelezo mengi kesho (leo), atakapokutana na waandishi wa habari makao makuu.

“Tuna mambo mengi mno, kumekuwapo na tatizo la viongozi wetu wengi kukamatwa kila kukicha maeneo mbalimbali, sisi kama chama cha upinzani hatuwezi kunyamazia jambo hili,”
 alisema Mrema.

Moja ya matukio ambayo yalitikisha nchi hivi karibuni ni kukamatwa kwa Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu, kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi  kuwa “Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli ni ya ubaguzi wa ufamilia,ukabila, ukanda na udini.”

Kutokana na tuhuma hizo, alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka ya uchochezi.

Baada ya kupewa dhamana Lissu alisema hakuna gereza likalowanyamazisha  na  kwamba wataendelea kuzungumza siku hadi siku hadi kifo kitakapowachukua.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment