Mahakama yatoa siku 7 kukamilisha upelelezi kesi ya Aveva na Kaburu


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetoa siku saba kwa upande wa mashitaka kufanya jitihada za kukamilisha upelelezi katika kesi inayowakabili vigogo wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Geofrey Nyange maarufu Kaburu.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mwendesha Mashitaka Mwandamizi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa ,(Takukuru), Leonard Swai kudai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika.
Upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Mtakyamirwa Philemon ulidai kuwa ni mara ya nne upande wa mashitaka unadai kuwa upelelezi haujakamilika na kwamba washitakiwa hao wanaongoza vyombo vikubwa ambapo shughuli zimesimama. Wakili Philemon alidai upande wa mashitaka unatakiwa kuhakikisha wanakuwa makini na shauri hilo ili wakamilishe upelelezi kwani washitakiwa wako ndani kwa kosa lisilo na dhamana.
Hata hivyo, Swai alidai anatambua kuwa washitakiwa ni viongozi wa timu kubwa lakini iliyoshitakiwa sio klabu bali ni wao binafsi. Alidai mashitaka ya kughushi wanahitaji upelelezi wa kina hivyo anaomba mahakama kuwapa siku 14 kwa sababu kuwaleta mara kwa mara washitakiwa Hakimu Nongwa alisema mahakama imezingatia hoja za pande zote mbili kwamba mashitaka ya kughushi yanachukua muda mrefu kukamilika.
Alisema mashitaka hayo hayapati haki ya kufutwa ndani ya siku 60 licha ya kuwa na dhamana, lakini mashitaka mengine ya utakatishaji fedha yanayowakabili hayana dhamana. "Hivyo hatujui ni lini upelelezi utakamilika kwa kuwa upande wa mashitaka umepewa muda mrefu wa kufanya upelelezi na mahakama haina mamlaka ya kufuta mashitaka hayo. Mahakama inatoa muda mfupi ili upande wa mashitaka ufanye jitihada y kukamilisha upelelezi," alisema Hakimu Nongwa.
Alisisitiza kuwa licha ya sheria kutaka kuahirishwa kwa kesi kusizidi siku 14, lakini ombi la upande wa utetezi linamaana hivyo tunatoa muda huo ili kama washitakiwa wakiwa na hatia watiwe hatiani. Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka ya kughushi na kutakatisha fedha. Inadaiwa Machi 15, mwaka jana, jijini Dar es Salaam, washitakiwa wote kwa pamoja walighushi fomu ya kuhamisha fedha kuonesha kwamba Klabu ya Simba inalipa deni la Dola za Marekani 300,000 kwa Aveva, kitu ambacho si kweli.
Katika mashitaka ya pili yanayomkabili Aveva, inadaiwa Machi 15, mwaka jana maeneo ya Benki ya CRDB tawi la Azikiwe wilayani Ilala, Dar es Salaam, alitoa nyaraka hiyo ya uongo kwa benki hiyo kuonesha kuwa Klabu hiyo inalipa Dola za Marekani 300,000 kwa Aveva.
Pia inadaiwa tarehe tofauti tofauti kati ya Machi 15 na Juni 29, mwaka jana, ndani ya mkoa huo, washitakiwa walikula njama kutakatisha fedha Dola za Marekani 300,000 huku wakijua kwamba fedha hizo ni zao la uhalifu ambalo ni kughushi.
Machi 15 mwaka jana, katika Benki ya Barclays Mikocheni wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, Aveva alijipatia Dola za Marekani 300,000 wakati akijua kuwa alipata fedha hizo kutokana na nyaraka za kughushi.
Katika mashitaka ya tano yanayomkabili Nyange, ilidaiwa Machi 15, mwaka jana katika tawi la Barclays tawi la Mikocheni, alimsaidia Aveva kupata fedha kutoka katika benki hiyo huku akijua kwamba ni zao la uhalifu ambalo ni kutokana na kughushi fomu ya kuhamishia fedha.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment